UVCCM WAITAKA SERIKALI KUFUNGIA MTANDAO WA X KULINDA MAADILI NA UTAMADUNI WA WATANZANIA


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) wameitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania 

"Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tumekua na Utamaduni lakini na Kazi ya Kufuatilia malezi ya Vijana wote, na hili Jukumu letu la Msingi, Kikatiba na Kikanuni kupitia Jumuiya yetu pendwa ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi". 

"Hivi Karibuni UVCCM tumepokea taarifa ambayo Vijana wa Chama Cha Mapinduzi imetushtua kidogo kupitia mtandao wa X  na sisi wengine tulianza kushtuka mapema kwanza jina lake kubadilika na kuitwa X maana yake tulikua tunaandali kisaikolojia Kwamba kila kitu kinachokuja ndani yake tuone ni cha kawaida"

"Sasa zetu hawa wametoa tangazo la kuruhusu kwamba  maudhui yote ya kingono na mengineyo ambayo kimsingi ukifuatikia Utamaduni na silka zetu hatuaendani nayo, tumeona Serikali imefungia Mitandao na Tovuti nyingine zinazorushwa maudhui hayo zimefungiwa, sasa ni wakati wa kufungia na huu wa X.

"Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunaitaka Serikali kupitia Wizara yake inayoongoza Mitandao ya Kijamii waugungia mtandao huu au kama wataweza kuondoa maudhui haya tupo tayari kuendelea nao" alisema hayo Komredi Kawaida

Aidha Komredi Kawaida ametoa wito kwa Viongozi  Vijana nchini ikiwemo Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Makatibu na Wenyeviti wa Umoja wa Vijana Wilaya na Mikoa yote nchini kutoka kwa pamoja kukemea kitu hiki ambacho kinataka kuletwa katika nchi yetu 

Post a Comment

Previous Post Next Post