Mdau wa michezo na Waziri wa Madini wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewataka magolikipa wazawa kushirikiana na kusaidiana katika kuendeleza vipaji vyao ili Taifa linufaike na huduma yao.
Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipowapokea magolikipa hao ambao wamemtembelea wakitoka Wilayani Kahama,Mkoa wa Shinyanga.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri ambayo kila mmoja wenu ameifanya katika Timu yake.
Jengeni utamaduni wa kupendana na kusaidiana katika kukuza vipaji vyenu,tunatamani kuwaona magolikipa wengi zaidi wa Kitanzania wenye uwezo mkubwa wa kushindana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania”Alisema Mavunde
Naye Mwenyekiti wa Magolikipa wa Tanzania Ndg. Juma Kaseja,amemshukuru Mh. Mavunde kwa ukarimu na kuwapokea ingawaje walitoa taarifa ya muda mfupi.
Ametumia fursa hiyo pia kueleza kuwa malengo makubwa ya umoja wao ni kushiriki katika shughuli za kijamii kwa kurudisha kwenye jamii,kushirikiana na kusaidiana katika kukuza vipaji vyao na kuondoa dhana kwamba magolikipa wa Tanzania hawapendani na kutakiana mabaya.