KATIMBA ATOA SIKU 3O KWA MKANDARASI UTEKELEZAJI MRADI WA TACTIC


NAIBU WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Mhe.Zainab Katimba amemtaka mkandarasi  Chongqing International  construction Corparation (CICO) kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana  ujenzi wa mradi wa Tactic

ili kufikia kiwango cha utekelezaji wa mradi kwa mujibu wa mkataba.

Ametoa maelekezo hayo leo juni 9,2024 alipotembelea  ujenzi wa barabara ya Swetu  inayojengwa kupitia mradi wa TACTIC katika Halmashauri ya  Manispaa ya Tabora,Mkoani Tabora.

Katimba amesema kwa mujibu wa ratiba mkandarasi huyo anatakiwa kuwa amefikia asilimia 40 ya  utekelezaji wa mradi lakini mpaka sasa amefikia  asilimia 8.6

'Tunataka kuona kasi ya ujenzi ili kufikia asilimia ya utekelezaji wa mradi iliyokubalika kwenye mikataba kwa kuwa mkifanya tofauti mnakuwa mmevunja mkataba' amesisitiza Katimba

Katimba ametoa siku 30 za matazamio kwa mkandarasi huyo  kuanzia juni 8,2024 ili kukamilisha utekelezaji wa miradi kulingana na ratiba iliyowekwa kwenye mkataba

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha kwa ajili ya kuwahudumia wananchi,hivyo ni jukumu la mkandarasi kuhakikisha anatimiza majukumu yake kimkataba.

'Hatubembelezi wala hatuombi kwa kuwa serikali imeshatimiza jukumu lake hivyo ni wajibu wa mkandarasi kukamilisha kazi kwa wakati kama ilivyokubalika kwenye mkataba,'" amesisitiza Mhe. Katimba

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora  Mjini Mhe. Deusdedit Katwale amemtaka mhandisi mshauri  UNITEC CIVIl  Consultants Ltd kuhakikisha anasimamia taratibu kwa kuwa yeye ndiye aliyewekwa na Serikali katika usimamizi wa mradi huo na kuchukua hatua kwa mkandarasi kwa mujibu wa sheria, taratibu na miongozo ya serikali.

Ameitaka Halmashauri ya manispaa ya Tabora kuhakikisha wanachagua wakandarasi wenye uwezo wa kazi na kuacha tabia ya kuchagua wakandarasi wwnye gharama ndogo. 

'Katika miradi mikubwa kama  hii ni vyema  tukaangalia uwezo wa mkandarasi, vifaa anavyotumia na umahiri wa kazi,tujiepushe kuchukua wakandarasi ambao gharama zao ni za chini ambao mara nyingi huchelewesha ukamilishaji wa miradi kwa wakati' amesisitiza Mhe. Katwale

Mhandisi  wa Wakala wa barabara vijijini na mijini  Subira Manyama amesema kuwa jumla ya shilingi bilioni 16.5 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 10.7.


Amesema,mkandarasi huyo ameingia mkataba wa ujenzi wa barabara ya mkunazini -madaraka Kanon kisarika,Malitano,swetu  ujenzi wa Jango la ofisi ya mhandisi ambavyo vote hivyo vimetekelezwa kwa asilimia 8.6


Aidha,Halmashauri ya Manispaa ya  Tabora ni miongoni mwa halmashauri 12 zilizoingia kwenye mradi wa TACTC kwa kigezo cha idadi kubwa ya watu na ukuaji wa miji kwa mujibu w sensa ya mwaka 2012

Post a Comment

Previous Post Next Post