TAASISI YA DORIS MOLLEL YAPONGEZWA KUFANIKISHA ONGEZEKO LA LIKIZO YA UZAZI


Serikali ya Tanzania imefanya uamuzi wa kihistoria kwa kuridhia ombi la Taasisi ya Doris Mollel la kuongeza likizo kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti. Hatua hii muhimu ilifanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, alipomwakilisha Rais katika Sherehe za Kilele cha Mei Mosi Kitaifa, Arusha. Likizo hii itaanza baada ya kumalizika kwa kipindi cha uangalizi wa maalum kwa mujibu wa madaktari.

Taasisi ya Doris Mollel, ambayo ilihamasisha wazo hili, inatoa shukrani za dhati kwa wadau wote walioshirikiana katika mchakato huu. Wadau hawa ni pamoja na wataalamu wa afya, wazazi wa watoto njiti, wataalamu wa sheria, na mashirika mengine yanayopigania haki za wanawake na watoto. Hatua hii pia imehusisha mapitio ya sheria za haki za mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati.

Taasisi ya Doris Mollel inawapongeza wadau wa maendeleo kama Women Fund Tanzania Trust, Asas Group, na Segal Family Foundation kwa mchango wao usiopimika. Shukrani pia ziwaende kwa waandishi vinara wa watoto njiti ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kupigania ajenda za watoto njiti.

Taasisi ya Doris Mollel iko tayari kushirikiana na wadau wote katika hatua zote za kuhakikisha kuwa uamuzi huu unajumuishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, kwa lengo la kuendeleza ustawi wa wanawake na watoto nchini Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post