GAVANA BWANKU AWAHIMIZA WANUFAIKA WA TASAF KATERERO, KUANZISHA MIRADI


Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyoko wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku Jana amekutana na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kwenye kijiji cha Kitahya, Kata ya Nyakibimbili ambapo amewahimiza wanufaika hao wa TASAF kutumia sehemu ya fedha wanazopata kila mwezi kupitia TASAF kuanzisha miradi midogo ya uzalishaji kama ufugaji, kilimo na biashara ili waweze kuimarisha kipato chao na kujitoa katika umaskini.


Kwenye kikao chake hicho na wanufaika wa TASAF, Gavana Bwanku aliambatana na Mtendaji wa Kata ya Nyakibimbili Ndugu Bashiru, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitahya Ndugu Kawili Elias, Mtendaji wa Kijiji Ndugu Mgala Masatu na wawezeshaji wa TASAF ngazi ya Kata ambapo amewaahidi kuwatafutia masoko ya bidhaa watakazozalisha kwenye miradi yao na kuwasaidia kuwaunganisha na Wataalamu wa miradi ili watekeleze miradi kwa tija huku akiwaeleza anategemea anayenufaika na TASAF baada ya muda mfupi aimarike kiuchumi na kujitoa kwenye TASAF ili Watanzania wengine wenye mahitaji wanufaike.


Gavana Bwanku amewaeleza wanufaika hao jinsi Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilivyotunisha zaidi mfuko wa TASAF na kufikia sasa Watanzania zaidi ya Milioni 5 kunufaika ili kuboresha maisha yao huku Bajeti ya TASAF sasa ikiwa zaidi ya Bilioni 400.


Pia Gavana Bwanku amewaeleza wanufaika hao wa TASAF  jinsi Rais Samia alivyomudu kuliongoza Taifa kwa miaka mitatu huku shughuli za maendeleo na miradi ya maendeleo ikienda kwa kasi zaidi na kuthibitishia Taifa na ulimwengu kwamba Wanawake ni Jeshi kubwa

Post a Comment

Previous Post Next Post