MOROGORO WAPO TAYARI KWA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA.RC MALIMA


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Alhajii Adam K. Malima amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya uratibu wa kufanikisha kambi ya madaktari Bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kanda ya kati ikihusisha Hospital za Rufaa Mikoa ya Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma  na Pwani .

Hatua hiyo ni katika kuhakikisha serikali inasogeza huduma za afya  karibu na wananchi, kwa kushirikiana na  Wizara ya Afya  ambapo kambi kubwa ya matibabu ya magonjwa kadhaa  linatarajiwa kuanza  Mei 6 - 10, 2024 katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa  Morogoro itayoshirikisha madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi kutoka Hospital za Rufaa kanda Taifa  ikiwemo Benjamini Mkapa Hospital, Jakaya Kikwete  Hospital,  Hospital ya Mifupa MOI  na hospital ya Muhimbili.

Aidha RC Malima pia alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa Habari kisha kutembelea ukarabati mkubwa unaondelea  katika hatua za mwisho  Hospital ya Rufaa Morogoro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufakisha kambi hilo.

"Nitoe wito kwa wakaazi wa Morogoro na mikoa yote ya jirani  kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kitabibu, tumejipanga vyema na wataalamu wetu kutoa huduma za wanawake, magonjwa ya watoto, magonjwa ya masikio, Meno, magonjw ya upasuaji wa mifupa, magonjwa ya upasuaji wa jumla, magonjwa ya ndani (Moyo, Figo, Ini, na matumbo, magonjwa ya afya ya akili, magonjwa ya ngozi,  magonjwa ya macho, huduma za ganzi na usingizi, magonjwa ya mfumo wa mkojo  huduma za uchunguzi za mionzi na picha, huduma za utegemao na mazoezi tiba ambapo huduma zote zitatokewa bila malipo"

"Tunamshukuru sana sana Dkt Samia Saluhu Hassan kwa wema, imani na ungwana wake kuhakikisha kila mtanzania anahudumiwa popote pale alipo sio jambo dogo kikosi cha wataalam Bingwa na Bingwa Bobezi zaidi ya 54 kupiga kambi na kuhakikisha kila mwenye tatizo la kiafya anafikiwa bila kujali gharama na ukubwa wa tiba anayohitaji huu ni zaidi ya upendo mkubwa tutahakikisha tunaitumia vyema fursa hii" Adama Kigoma Malima RC Morogoro

Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya, Mbunge wa Jimbo la Kilombero  Asenga Abuubakari kwa niaba ya wabunge wa majimbo ya mkoa wa Morogoro, madaktari wandamizi wa Hospital za Rufaa mikoa ya kanda ya kati, watumishi wa Hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro pamoja na waandishi wa Habari kutoka vyombo mabli mbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post