Mbunge wa Jimbo la Pangani ambae pia ni Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amewaongoza wana Pangani katika dua maalum ya kumuombe kheri na baraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ilioendana sambamba ni Iftrar ya pamoja ya wananchi wa Wilaya ya Pangani.
Akizungumza na viongozi na maelfu ya wananchi waliojitokeza Kata ya Mwera amewasihi kuendelea kudumu katika upendo kuwa na umoja, mshikamano na ushirikiano kwani huo ndio msingi wa mafanikio na maendeleo.
Amewahakikishia kuwa kazi kubwa itandelea kufanyika kumaliza miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa jimboni Pangani.
Aidha tukio hili limehudhuriwa na mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Batilda Buriani.
Pamoja na viongozi wengine wengi wa serikali ya Mkoa na Wilaya pia amehudhuria Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Ndugu Rajabu Abdulaman.
