MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amekutana na kusikiliza kero mbalimbali akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama wilayani Tarime mkoani Mara.
Kinana amewasili wilayani humo akitokea Wilaya ya Serengeti alikoanzia ziara yake na baada ya kuingia Wilaya ya Tarime alihudhuria kikao maalumu cha ndani cha CCM Jimbo la Tarime Vijijini kilichofanyika eneo la Nyamwaga katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Tags
Siasa