WATENDAJI SERIKALINI ACHENI VISINGIZIO KATIKA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI - AWESO.


Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amewataka watendaji wa serikali kuacha visingizio katika kipindi cha matatizo badala yake washirikiane katika kutatua matatizo. 

Mhe. Aweso ameyasema hayo siku ya leo tarehe 23 Feb akiwa Bwawa la Kidatu mkoani Morogoro alipojumuika katika ziara ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko kutembelea mabwawa ya kufua Umeme ya Kihansi na Kidatu pamoja na kuyaagiza mabonde yote tisa nchini kuhakikisha vyanzo vya vinatunzwa na kuhifadhiwa vyena viweze kitiririsha Maji ipasavyo kwenye Mabwawa ya uzalishaji wa Umeme.

Waziri Aweso amewataka watendaji kushirikiana katika kutunza vyanzo vya maji kwani matatizo yanapokuja yanasumbua Wananchi wote, suala hili ni mtambuka kwa Sekta zote Kilimo, Nishati, Mazingira na Mifugo watendaji hawana budi kushirikiana katika utunzaji wa vyanzo vya maji kwa pamoja. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dotto Biteko ameridhishwa na hali ya ujazo wa Maji katima Mabwawa haya na kuwahakikishia watanzania kuwa ndani ya kipindi cha mfupi hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika itakua sawa.

“Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwisha toa rasilimali zote Umeme upatikane sisi watu wa Wizara ya Maji hatutakuwa kikwazo kwa upatikanaji wa umeme kwa kusimamia vyanzo vya maji ili maji yaweze kujaa katika mabwawa ya kuzalisha Umeme kwani Umeme unategemea Maji na Maji ili yasukumwe kwa wananchi yanategemea Umeme.


Post a Comment

Previous Post Next Post