TOENI ELIMU YA SARATANI KWA WANANCHI; DKT NDUNGULILE


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi imetoa  rai  kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuongeza kasi  ya utoaji elimu ya ugonjwa wa Saratani kwa jamii ili kuchukua tahadhari na kuwahi matibabu kwa wakati.

Rai  hiyo  imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Februari 23, 2024 akiiongoza Kamati hiyo kufanya ziara ya kuona hali ya utoaji huduma za Afya, maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma ikiwemo na miradi ya afya inayotekelezwa na Taasisi hiyo.

Dkt. Ndungulile amesema kuwa  jamii  ikiwa  na elimu  ya kutosha  juu  ya ugonjwa wa Saratani watapata  muamoko wa kuwahi  Hospitali na kupata  matibabu sahihi  kwa wakati. 

"Hivyo  kuna haja ya kutanua  huduma za Saratani kuwa zinapatikana katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na Kanda ili  kupunguza adha ya wananchi  kusafiri mwendo  mrefu na kutumia  gharama kubwa kufata  huduma hizo Dar es Salaam.   

Audha ameipongeza  Taasisi hiyo  kwa kuboresha miundombinu na kuwa  wabunifu  katika  kuzalisha  mionzi  tiba  itakayotumika nchi  nzima na Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza  fedha  nyingi katika sekta ya afya  na kuifanya  Tanzania kitovu cha  tiba utalii Afrika Mashariki .

"Uwekezaji  huu  mkubwa  alofanya  Dkt Samia unalenga  kuinufaisha  nchi  katika  kuongeza  pato la taifa kwani  tutapata  fedha za kigeni  kwa kwa  kuwauzia nchi  jirani  mionzi  inayozalishwa  hapa Ocean Road ", ameeleza  Dkt Mollel

Post a Comment

Previous Post Next Post