Maafisa Habari Serikalini wameagizwa kutangaza miradi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili wananchi wajue ikiwemo kujibu hoja za uongo zinazotolewa na watu dhidi ya serikali .
Akifungua Mkutano wa siku tatu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano
Serikalini(TAGCO) Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Dk,Damas Ndimbaro
kwaniaba ya Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko.
Alisema maofisa hao wanawajibu mkubwa wakutangaza shughuli mbalimbali
zinazofanywa na serikali ili watu waone ukubwa wa kazi zinazofanywa na serikali
katika nchi hii
"Baadhi ya watu hawaoni ukubwa wa katarasi nyeupe ulivyo sasa ni
wajibu wenu kueleza kazi zinazofanywa na serikali ikiwemo kujibu hoja za uongo
dhidi ya serikali lazima mjue kujibu fitna na zengwe"
Alisema hata serikali inapigwa fitna sasa ni kazi yenu kujibu fitna na
zengwe kwani hivi sasa zama za teknolojia ya habari imekua na ni nzuri ila
inachangamoto zake kupitia mitandao ya kijamii.
Alisema mojakati ya changamoto kubwa iliyoletwa na mitandao ya kijamii
haijui ni nani mtoa habari na nani anayepaswa kujua hii ni habari hivyo tumieni
changomoto hizi kwaajili ya kujibu hoja na lazima mafunzo ya mara kwa mara
yatolewe ya matumizi ya mitandao ya kijamii
"Ongezeni ubunifu zaidi,msifanye kama jana kazi zenu maafisa habari
ili muweze kupambana zaidi na kuipambania serikali "
Alitoa rai kwa waandishi wa habari vyombo vya serikali na
maafisa habari kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uzalendo,weledi na
ubunifu pale taarifa zinavyoandikwa
Alitoa maelekezo kwa waaajiri wote wasioweza kuleta maafisa habari
kushiriki mkutano huo watoe maelezo kimaandishi na ifikapo mwakani Maafisa wote
wa serikali na wasio wa serikali wajiunge na chama hicho
Alisema treni ya majaribio ya umeme imeanza kazi kwa majaribio ingawa
kulikuwa na kebehi nyingi sana lakini treni imeshaanza kazi hivyo serikali
inafanya kazi kwa vitendo
Aliwasihu maafisa hao kujiunga kwa pamoja kutetea serikali pale jambo
linapotokea badala ya kuachia wizara husika pekee kutoa ufafanuzi ikiwemo kutoa
hamasa kwa wananchi kujua umuhimu wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa
ikiwemo utangazaji wa miradi ya kimkakati ya serikali
Huku Msemaji Mkuu wa Serikali,Mobhare Matinyi alisema baadhi ya
halmshauri hazina maafisa mawasiliano wa serikali badala yake maofisa Tehama
ndio wanaongoza kitengo hicho hali inayokwamisha hali ya wananchi kupata
habari.
"Halmashauri 180 zilizopo nchini lakini inashangaza kuona baadhi yao
siwezi kutaja idadi hazina maafisa habari na hawajui maana ya habari na
ukiuliza sababu gani hakuna maafisa habari unajibiwa majibu
yasiyorithisha"
Lakini pia kwenu maafisa mawasiliano ya serikali wapeni nafasi nao wananchi
wazungumze kuhusu mambo mbalimbimbali yanayowasibu ila pia ni lazima sasa
halmashauri ziajiri maafisa habari ili waweze kusemea vema serikali na wananchi
kupata habari zaidi
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari na Teknolojia na Mawasiliano,
Selestine Kakere alisema wizara inatekeleza kutangaza sera,kanuni na taratibu
ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambapo kazi za serikali
kwa Umma zinafanyika kupitia mitandao ya kijamii,radio na luninga
Alitoa rai kwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya ambao mikoa yao Haina
maofisa habari wafanye hima kuajiri maofisa habari katika mikoa yao stahiki
Alisema mikoa 14 imepata fursa ya kutangaza miradi mbalimbali ya serikali
huku zoezi hilo likiwa linaendelea ikiwemo uwekaji misingi ya uhuru wa vyombo
vya habari sanjari na kushamiri kwa idadi kubwa ya vyombo vya habari ikiweo
magazeti ,radio na televisheni za mitandao,blogu .
Alisema uwepo wa baadhi ya Wanahabari wengine wasio na weledi na sifa za
wanahabari lakini bodi ya ithibati ipo katika hatua ya uanzishwaji ili kusaidia
kuimarisha weledi katika sekta ya habari nchini huku baadhi ya
taasisi za mawasiliano kwa umma baadhi hazitekelezi majukumu yake.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Joshua Nassari alisema ushirikoshwaji wa
maofisa mawasiliano ni chachu ya kutoa taarifa kwa umma na kuongeza kuwa
wamepokea agizo lakila halmashauri kuwa na maofisa habari na mikoa kwa ujumla
Awali Kaimu Mwenyekiti wa TAGCO, Karim Meshack
alisema chama hicho kitaendelea kuhakikisha kinawunganisha maafisa habari
kujadili mambo mbalimbali sanjari na kujifunza mbinu mbalimbali za teknolojia
za upashanaji habari.