MAPOKEZI YA WAJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJAI YA UVCCM TAIFA MKOANI MANYARA


Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapainduzi Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC)  wamewasili Mkoani Manyara na kupokelewa na Viongozi pamoja na Wanachama Mkoani humo tarehe 19 Februari, 2024.

Viongozi hao wamewasili mkoani Manyara kuanza Ziara ya kikazi katika Wilaya zote za mkoa huo.

Lengo la Ziara hio ni kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya 6, kukagua Uhai Chama na Jumuiya zake, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Vijana na wananchi kwa Ujumla pamoja na kuhamaisha ushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na kuwasihi  wanachama na wananchi wote kuchagua wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikaki za Mitaa 2024

Post a Comment

Previous Post Next Post