Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso leo tarehe 27/02/2024 akishiriki ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Mara Mhe Kassim Majaliwa amempa maelekezo mahususi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mgango-Kiabakari-Butiama ndani ya wiki mbili kufungulia Maji yaanze kuingia kwenye matenki ili wananchi wa Butiama wapate huduma ya maji.
Mradi wa maji Mgango-Kiabakari-Butiama una gharimu Bilioni 70.5 mpaka kukamilika na kwasasa mradi huo upo asilimia 97 na upo tayari kuanza kuwahudumia wananchi.
Waziri Aweso ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama kusalimiana na Wananchi wa Wilaya ya Butiama.
Aidha Mhe Waziri Mkuu amesema kuwa wananchi wa eneo hilo, maji wanayoyatumia ni mradi ambao ni wa muda mrefu sana na unazalisha maji ambayo sio toshelezi kwa mahitaji ya wakazi hao na nduo sababu Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan iliwekeza pesa nyingi kiasi cha Bil.70.5 na kuanza ujenzi wa mradi mkubwa na wa kihistoria utakao maliza kabisa changamoto ya Maji katika mji wa Butiama