Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva ameelekeza kuwa mpaka kufikia siku ya Jumatatu tarehe 15 mwezi January wazazi wote wenye watoto wanaotakiwa kuanza Kidato cha kwanza, Darasa la kwanza na Awali kuhakikisha wanawapeleka shuleni watoto hao kuanza masomo haraka iwezekanavyo kwani timu yake itakapopita kukagua na kuwakuta watoto hao majumbani hatukuwa na mdhamana na mtu.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa tamko hilo alipofanya ziara ya kutembelea shule mbalimbali wilayani humo ili kuona kasi ya watoto kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali ambao tayari wameripoti ndani ya wiki moja ya ufunguzi wa shule na kukuta idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza bado hairidhishi ambapo kwa Wilaya nzima wameripoti asilimia 60 pekee hiku asilimia 40 wakiwa bado hawajatipoti huku kwa darasa la kwanza na awali wakitipoti zaidi ya asilimia 85.
Katika hatua nyingine Mwanziva amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza nguvu katika kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa na madawati hivyo wazazi wanapaswa kuungana na serikali katika kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni ili waweze kupata elimu iliyo bora.
"Nimesikia wazazi wanasubiri siku za ya mnada/guluo ili wawanunulie watoto wao mahitaji na kuwaleta shuleni, sasa wiki hii ndilo wiki ya mnada katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu- wajitahidi wakamilishe mahitaji, na kwa wale watakaokwama sisi hatuna kipingamizi au masharti yoyote tunachotizama ni watoto kuripoti mashuleni kwanza, ninaomba kwanzia Jumatatu ya Tarehe 15 January kila mtoto awe ameripoti shuleni kuanza masomo".
Tags
Habari