WAZIRI AWESO AMPA TANO RAIS MWINYI KASI YA MAENDELEO ZANZIBAR


Waziri wa Maji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jumaa Aweso leo Tarehe 31 December 2023 amezindua Mradi wa Maji wa Tangi la Chanjaani Chakechake PEMBA ikiwa ni sehemu za shamrashamra kuelekea Maadhimisho ya sherehe za miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Mradi huu utawanufaisha wananchi wa vijiji vinne vya Chanjaani, Madungu, Fueni na Kilimni.

Waziri Aweso amempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi kubwa aliofanya ya kuwaletea wananchi maendeleo hususani katika ujenzi wa Miundombinu na huduma za jamii mfano ujenzi wa Miradi ya Maji.
Amesisitiza kuwa Chini ya Rais Mwinyi ndani ya muda mfupi Zanzibar imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo na kazi kubwa inaendelea kufanyika.

Aidha Waziri Aweso amempongeza Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kazi kubwa aliofanya kupitia Mamlaka ya Maji ya Zanzibar ZAWA katika kutekeleza na kukamilisha ujenzi wa Mradi huu mkubwa wa Maji.

Mwisho Waziri Aweso ametoa salam za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi akiwaeleza kuwa anawasalimu sana na anawahimiza kuendelea kushirikiana na kushikamana, kulinda na kuitunza amani yetu, kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kuiunga mkono serikali yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post