TAHOSSA YAWASHIKA MKONO WAATHIKA WA MAFURIKO HANAN


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na elfu thelathini na nne na senti hamsini (2,034,000.50/) kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ikiwa ni mchango kutoka Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya matope na mawe kutoka mlima Hanang.

Mhe. Mchengerwa amekabidhi fedha hizo Leo 19 Disemba Ofisini kwa Waziri Jenista Jijini Dodoma, ambapo amepokea fedha hizo kwa Niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema TAHOSSA wakati wanahitimishi Mkutano wao wa 18 pamoja na mambo mengine mengi waliyofanya wametoa mchango wao kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwahudumia wanzetu wa Hanang waliopatwa na janga la mafuriko.

Amesema Wakuu wa Shule za Sekondari kwa ushirikiano wao Waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang’ na kunituma nikukabidhi wewe Waziri mwenye dhamana.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema  Jambo hili la maafa la maporomoko ya Matope na Mawe kutoka Mlima Hanang’ amesema Walimu ni Viongozi,na wamedhihirisha uongozi wao katika mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuunga mkono katika masuala mbalimbali hususani ni hili mafuriko ya Hanang.” Mhe. Mhagama.

Alisema Serikali imeendalelea kuhakikisha kuwa inarejesha hali ya kawaida kwa wananchi wa Hanang na mafanikio yote yalipatikana yameongozwa na utashi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

Previous Post Next Post