SERIKALI KUTOA MAGARI 3 YA AMBULANCE NA KUJENGA KITUO CHA AFYA HANANG


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na timu kutoka Wizara ya Afya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wametembelea eneo lililoathirika na maporomoko ya matope yaliyopelekea vifo vya watu 89 na majeruhi 139 Wilaya ya Hanang Mkoni Manyara. 

Katika ziara hiyo Waziri Ummy amebainisha mambo kadhaa yatakayoendelea kutekelezwa na Serikali ikiwemo kupeleka magari Matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance), kujenga kituo cha Afya katika eneo lililotengwa na Serikali kwa makazi ya watu.

“Serikali itaendelea kuwahudumia majeruhi waliobakia kwa sasa ambao ni Watano kwa gharama za Serikali Kama alivyoelekeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.” Amesema Waziri Ummy.

Post a Comment

Previous Post Next Post