MHE. MAWAHANGA AWAASA MABINTI KUKWEPA MIKOPO KAUSHA DAMU.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mahawanga Janeth amekutana na Umoja wa Mabinti wa kidigitali wenye Wanachama 300 wanaoendesha umoja wao kwa njia ya whats app na kuuza biashara zao kupitia mitandao ya face book, instagram na tiktok kutoka Mikoa tofauti tofauti wanaojulika kwa jina la Unique Group.

Lengo la umoja huu ni kuondokana na adha ya mikopo kausha damu baada ya kuona changamoto ya kupata mitaji bila riba na kuitumia changamoto hiyo kama fursa ya wao kuanzisha umoja huo ambao wanauita mkakati wa kukusanya mtaji na kuanza na walicho nacho.

Mhe. Mahawanga amewapongeza sana Mabinti wa Unique kwa ubunifu na ujasiri mkubwa wa kuweza kusave kidogo kidogo kuanzia kiasi cha shilingi 2,000 kila wiki kwa mwaka mzima na kupeana maarifa mbalimbali ya ujasiriamali hali iliyopelekea kutengeneza ajira miongoni mwao sambamba na kumiliki biashara kupitia mitaji hiyo.  

Mhe. Mahawanga amefurahishwa sana na ubora wa biashara za Mabinti hao hasa bidhaa zinazotengenezwa kwa mikono yao. Lakini pia amewaambia bado wananafasi ya kukuza mitaji yao na kuongeza ukubwa wa biashara zao kupitia mikopo ya Halmashauri ya 4% kwa kundi la Vijana.

Mhe. Mahawanga ameendelea kutoa wito kwa Mabinti na Wanawake kuendelea kutumia mitandao ya kijamii kwa njia sahihi inayowaingizia kipato na kutengeneza ajira katika jamii.

Mwisho Mhe. Mahawanga amewaahidi Mabinti hao kushirikiana nao kuhakikisha ndoto zao zinatimia na kuendelea kushikana mikono kuhakikisha umoja huo unakuwa chachu kwa Mabinti wengine waliokata tamaa na kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa. 


Post a Comment

Previous Post Next Post