Wabunifu wa mavazi nchini walioshikiriki katika Maonyesho Makubwa ya Mavazi yanayojulikana kama “Swahili Fashion Week”walionyesha ubunifu wao wa mavazi mbalimbali maalumu yatakayoweza kuvaliwa na wazazi (Mama au Baba) watakaopata kabla ya wakati yaani Mtoto njiti na kuweza kumlea vizuri akiwa hospitalini na hata baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitalini.
Maonyesho hayo ambayo kilele chake ni leo yanafanyika katika ukumbi wa Bravo Coco ulioko katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es salaam ambapo Jumla ya mavazi 12 ya kumsaidia Mtoto njiti yameonyeshwa.
“Tunamshukuru sana muandaaji wa Maonyesho haya, Mustapha Hassanali kwa kutupa nafasi ya kuwapa hamasa wabunifu wetu kuja na ubunifu wa vazi hili, kikubwa kwetu ni kuelimisha jamii kupitia makundi mbali mbali na leo tumeifikia Tasnia hii ya Mitindo inayowagusa watu wengi wakiwemo vijana” - Doris Mollel - Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation.