WATENDAJI WA KATA NA MAAFISA TARAFA MSIKWEPE MAJUKUMU YENU-MHE MURAGILI


Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amewataka Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa kutokukwepa majukumu yao  kwa kuwa wao  ni sehemu ya Serikali  na  wanapaswa kujua nafasi walionayo katika maneo wanayotoa huduma.

Ameyasema hayo leo  wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Maafisa Watendaji wa Kata na Tarafa wa Mkoa wa Singida kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambapo mafunzo  hayo yanalengo  la kuwakumbusha utekelezaji wa majukumu yao kwenye maeneo  yao.


Amekemea tabia ya  baadhi ya maafisa  hukwepa majukumu yao  na kuchagua kazi za kufanya na  wakati mwengine kutoa lawama kwa Serikali huku wakisahau kuwa wao ndio wawakilishi wa  Serikali na wamewekwa hapo ili kuwahudumia wananchi .


“mnajisahau kuwa nyie ndio  Serikali wa eneo husika mnalofanyia kazi mnapaswa kushughulikia kila sekta kama elimu, miundombinu, afya, kilimo,uvuvi, amani, usalama, michezo na maafa yote haya mnapaswa kushughulika nayo"

Mhandisi Muragili amewataka  maafisa hao  pindi  mafunzo yatakapomalizika  watakuwa wamejifunza na kuenda kufanyia kazi kwa kufanya maamuzi kipi wanapaswa kushughulikia katika ngazi zao.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais- TAMISEMI Hamisi Mkunga amewakumbusha maafisa hao kuenda kuyafanyia kazi yale yote waliofundishwa kwa kuwa  mada zilizofundishwa zinaenda sambamba na utekelezaji wa majukumu  yao hivyo hakutakuwa na kisingizio cha kutokufanya kazi  kwa sababu ya kutokujua Sheria, Taratibu na Kanuni   na miongozo.


“mafunzo haya mliopatiwa mkatekeleze kwa vitendo tutawapima” amesisitiza Mkunga

Post a Comment

Previous Post Next Post