RAIS KIKWETE : MOLLEL FOUNDATION IMEFANYA MAKUBWA KUSAIDIA WATOTO NJITI NCHINI


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la Doris Mollel Foundation linalojihusisha na kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya Wakati Nchini kwa kugawa vifaa tiba kwa watoto njiti, kutoa elimu kwa umma kuhusu watoto njiti na kuhakikisha watoto njiti wanaishi wakipatiwa mazingira bora. 

Rais Mstaafu Kikwete ameyasema hayo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto aliyezaliwa kabla ya Kukamilika Wiki 37 za Umri wa Mimba leo tarehe 17, Novemba 2023 yaliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam yenye kauli mbiu ya "Hatua kidogo, Faida kubwa, huduma ya Ngozi kwa Ngozi, kwa Kila Mtoto, kila mahali" 

Rais Mstaafu Kikwete ameyasema pia ametoa wito kwa wajawazito kuhudhuria Kliniki kwa wakati ili wapate huduma na elimu stahiki 

"naomba nitoe rai kwa wajawazito wote kwamba wahudhurie kliniki ipasavyo ili wapate elimu na huduma stahiki, wajifungulie kwenye vituo vya kutolea huduma na wahudhurie kliniki baada ya kujifungua"

Pia Rais Mstaafu Kikwete ametoa wito kwa Serikali na wadau mbalimbali kuanzisha wodi kwa ajili ya watoto wachanga 
"Naomba nirudie tena ushauri kwamba; Mikoa, Halmshauri na wadau, ihakikishe kuwa  wodi za watoto kwa ajili ya huduma za Watoto wachanga (NCU) zinaanzishwa kwenye Hospital zote kama ilivyoelekezwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa takwimu za TDHS&MIS za 2022."

Post a Comment

Previous Post Next Post