Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC), Mwalimu Paulina Mkwama amesema kupitia Mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi (BOOST) vimenunuliwa vitendea kazi ikiwamo kompyuta mpakato 159 kwa gharama ya sh.milioni 375.
Mkwama ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi gari, pikipiki na kompyuta mpakato kwa ajili ya Katibu Wasaidizi wa Tume iliyofanyika leo kwenye Shule ya Sekondari ya Tambaza mkoani Dar es salaam.
"Mhe. Waziri tuna mfumo wa kielektroniki wa Tume ambao usaidia kuhifadhi na kuchatakata taarifa mbalimbali za walimu nchini na ili Makatibu Wasaidizi waweze kuutumia vizuri ni vyema wapatiwe vitendea kazi ambavyo ndio hizi Kompyuta Mpakato hivyo kwa sasa tutakua na uhakika wa upatikanaji wa taarifa safi za Walimu kutoka kwenye Halmashauri zote nchini,"amesema.
Katika Hafla hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe.Mohamed Mchengerwa amekabidhi gari moja aina ya Toyota Coaster, pikipiki 62 pamoja kompyuta mpakato 159.
Tags
Habari