Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)imeishauri Ofisi ya Rais - TAMISEMI kujenga, kusimamia na kufuatilia utekelezwaji wa ujenzi wa miradi ya elimu ihakikishe ujenzi huo uendane sambamba na utoaji wa elimu bora.
Kauli hiyo imetolewa Oktoba 28, 2023 wakati kwenye ziara yenye lengo la kukagua miradi ya elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Nyamagana Mkoani Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati Makamu Mwenyekiti Mhe.Justin Nyamoga amesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika elimu na inaendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu hivyo ni vyema walimu wakajikita katika utoaji wa elimu bora nchini.
Amesema pamoja na uwekezaji huo Wizara ya TAMISEMI pamoja na mipango yake mengine lakini pia iendelee kuongeza miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kwa walimu pamoja na vifaa vya kufundishia.
Kamati ikatoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuhakikisha wanasimamia na kushughulikia eneo linalotarajiwa kujengwa kituo cha mafuta karibu na shule hiyo ili eneo hilo libaki kuwa la shule kwa ajili ya usalama.
Kwa upande wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni usimamizi madhubuti wa uongozi unaongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluh Hassan kwa kuitekeleza Ilani ya CCM kwa kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi wote.
Amesema miradi hiyo inatekelezwa nchi nzima na Mhe. Rais ametoa zaidi ya tshs. Bil.7.9 kuboresha elimu ya Sekondari na zaidi Bil.12 kuboresha elimu ya Awali na msingi.
Tags
Habari