Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) pamoja na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), wamewasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi, leo Oktoba 01, 2023.
Mawaziri hao wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa Mbeya, Mhe. Juma Homera katika ofisi yake na wataendelea na ziara katika wilaya ya Busokelo.
Katika ziara hiyo, watakagua mradi wa barabara ya Katumba - Mbambo- Tukuyu; Lot 3: Katumba - Lupaso (Kilometa 35.3) na Mbaka- Kibanja (Kilometa 20.7) pamoja na kufanya mkutano wa kuzungumza na wananchi Kandete mjini.
Tags
Habari