CHUO KIKUU INDIA KUMTUNUKU SHAHADA YA HESHIMA RAIS SAMIA' - J. MAKAMBA


Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba aliyepo Nchini India akiwa njiani kumpokea Rais Samia amesema Chuo Kikuu cha India kimesema kitamtunuku shahada ya heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Makamba amesema chuo hiko kikuu cha Jawaharlal Nehru University kilichopo Delhi Nchini India kimefikia uamuzi huo baada ya kutambua mchango wa Rais Samia kwenye kuunganisha nchi hizi mbili (India na Tanzania) 

'Tumepata taarifa rasmi kuwa Chuo Kikuu kinachoheshimika hapa India cha Jawaharlal Nehru kimeamua kumtunuku Rais wetu Shahada ya Udaktari ya Heshima.”

Chuo hiki ni namba moja wamesoma watu muhimu hapa akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje [wa India] sasa hivi, Waziri wa Fedha na wengine wengi. Wameamua kufanya hivyo kwa kutambua mchango wake katika diplomasia ya uchumi, mafanikio katika kusukuma maendeleo yanayogusa watu moja kwa moja katika nchi yetu na mafanikio katika kuimarisha mahusiano ya Kimataifa kwa ujumla kwenye Umoja wa Mataifa.” 

Post a Comment

Previous Post Next Post