WAZIRI PROF. KITILA ABAINISHA KUWA MKAKATI MKUBWA NI KUVUTIA UWEKEZAJI MKUBWA NCHINI.


Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo Amesema kuandaliwa kwa kongamano la Kongamano la Uwekezaji na Biashara baina ya Tanzania na China ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza suala la kuvutia wawekezaji nchini.

Ameyasema hayo Septemba 25, 2023 wakati wa kufunga Kongamano la Uwekezaji na Biashara baina ya Tanzania na China lililodhaminiwa na Jimbo la Zhejiang (Jinhua) lililofanyika kwenye hoteli ya Rotan jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Kongamano hilo, alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana Mhe. Kassim Majaliwa

Prof. Kitila ameeleza kuwa, Ajenda kubwa ya Rais Samia, ni kujenga uchumi wa kisasa ambao umejengwa katika msingi wa Viwanda, kwani kupitia viwanda kutaleta ustawi kwa wananchi.

"Ili kufikia hatua hiyo, mkakati mkubwa ni kuvutia Uwekezaji mkubwa, wenzetu wachina wameitikia wito huu na kwakweli katika wiki hizi mbili tunashuhudia uwekezaji mkubwa kutoka kwa wenzetu"

Ametumia fursa hiyo kuelezea kuhusu Hatua za Ujenzi wa SINO TAN industrial park ambayo ni Hifadhi ya Viwanda iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani kuwa unaendelea vizuri na wanakwenda kwa kasi kubwa.

Amesema Hifadhi hiyo ya Viwanda linatarajiwa kuwekezwa Viwanda takribani 200 ambavyo vyote kwa pamoja Thamani yake ni Dola za Kimarekani Bilioni 3(sawa na Tsh. Trillioni 8) na kitazalisha Ajira Laki moja.

"Tayari baadhi ya Viwanda vimeshaanza kuchukuliwa na Wawekezaji kwa wingi wake" Amesema Prof. Kitila

Post a Comment

Previous Post Next Post