Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Four Seasons jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Tanzania ikiwa mwanachama wa WTTC itaendelea kujitangaza Kimataifa na itapata fursa ya kuwa mjumbe katika nafasi mbalimbali.
Baraza hilo lina mtandao wa mashirika binafsi zaidi ya 200 Duniani wanaotoa huduma mbalimbalia zenye lengo la kukuza utalii.
Aidha, katika kuendelea kutangaza utalii na kutafuta masoko mapya ya utalii, Mhe. Kairuki amefanya mazungumzo na wadau wakubwa wa utalii duniani ikiwa ni pamoja na Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia, Abdulrahman Alabdulwahab kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuitangaza Tanzania kupitia ndege za shirika hilo na kushirikiana katika kutangaza vivutio vya Utalii nchini.
Pia, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa City Sightseeing World wide, Enrique Ybarra kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuweka matangazo ya vivutio vya Tanzania kwenye vyombo vyake vya usafiri, na katika tovuti maarufu duniani ijulikanayo kama Isango.