MH. MAHAWANGA ASHIRIKI UZINDUZI WA MPANGO WA MRADI WA KIWANDA CHA USHONAJI TAWI LA KISANGA KATA YA WAZO



Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Mahawanga Janeth ameungana na mamia ya Wanawake wa Tawi la Kisanga Kata ya Wazo kuzindua mpango wa uanzishwaji Kiwanda cha ushonaji kama mradi wa Tawi hilo katika kujikwamua kiuchumi.


Katika uzinduzi huo lilifanyika tukio kubwa la kuwapokea Wanachama wapya wa UWT ambao wengi wao wanafurahishwa na kazi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi sambamba na fursa mbalimbali zinazowalenga Wanawake katika masuala mazima ya kuwainua kiuchumi.


Mh. Mahawanga amempongeza Rais Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayofanya lakini pia kurudisha fursa ya mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu na kuwataka wanufaika hao kuchangamkia fursa hii sambamba na kubuni miradi yenye tija ambayo itapelekea pesa hii kutopotea badala yake kutengeneza ajira na kuinua vipato vya Watanzania.


Lakini pia Mh. Mahawanga amewataka Wanawake wote kutoka Matawi 14 yanayounda Kata ya Wazo kuhakikisha kila Tawi linakuwa na mradi ili waweze kujitengenezea ajira miongoni mwao na kuondokana na utegemezi. Vile vile amewataka Viongozi kuwa wabunifu hata kama niwa ngazi ya Tawi kwani wananafasi kubwa ya kuionyesha jamii kile walichonacho hata kama wanaongoza ngazi ya Matawi.


Lakini pia Mh. Mahawanga amewataka Wanawake kuhakikisha wanaungana katika kutafuta maendeleo ya pamoja na kuwahakikishia

kuwakutanisha kwenye vikao vyao na wadau muhimu wa maendeleo kama Sido, TBS, Kampuni za Bima, Taasisi za Kifedha, Brella, TIC, Maafisa Biashara wa Halmashauri na Wataalam wa Masoko ili kuwapa uelewa mpana wakati wakiendelea na taratibu za kukamilisha mradi huo.


Na mwisho Mh. Mahawanga amewasisitiza Wanawake kuendeleza upendo na mshikamano katika safari ya kuelekea kwenye chaguzi zijazo lakini pia kugombea nafasi mbalimbali bila woga. Vile vile amewahikikishia Wanawake wa Tawi la Kisanga kuwa nao bega kwa bega mpaka mradi wao utakapokamilika kwani kiu yake ni kuona maendeleo makubwa ya Wanawake ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.


Post a Comment

Previous Post Next Post