Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 20/8/2023 amefanya ziara Kata ya Maweni pamoja na kufanya mkutano wa hadhara katika kata hiyo kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM katika katika Kata hiyo na Jimbo la Tanga Mjini.
Wakihutubia Mkutano huo Mhe. Ummy pamoja na Diwani wa Kata ya Maweni Mhe Joseph Colyvas waliwaeleza wakazi wa Maweni kuwa ndani ya miaka miwili na nusu hususani chini ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wametekeleza ahadi zao ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Ummy Mwalimu, ujenzi wa madarasa, kuimarisha huduma za Afya, Maji na Umeme sambamba na Ukarabati wa barabara za ndani za kata hiyo ambapo jumla ya shilingi *bilioni 1.7* zimetumika. Fedha ni nje ya fedha zilizotumika kuboresha bandari ya Tanga ambayo imeongeza fursa za kiuchumi kwa watu wa TangaMjini.
Aidha Mhe Ummy amesema tayari fedha za ujenzi wa km 2 za barabara ya lami katika kata hiyo zimeshaingia na tayari mchakato wa ujenzi umeshaanza. Pia, zaidi ya shilingi bilioni 2 zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha huduma za maji katika mitaa ya kata hiyo. Vilevile, Mhe Ummy amesema tayari mitandao ya simu miwili imeshafika katika Kata hiyo hatua itakayorahishisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu Maweni hususani maeneo ya Kichangani.
Kabla ya kuanza kwa Mkutano wa hadhara, Mhe. Ummy alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ya Kata ya Maweni ikiwemo kuzindua Kisima cha Maji Shule ya Msingi Kasera kilichojengwa na Tsiyon Urban Development NGO na Kisima cha Maji Maweni Sekondari kilichojengwa na Nyota Foundation ambapo Mh Ummy aliwashukuru wadau hawa kwa kuwaunga mkono watu wa TangaMjini.
Kabla ya Mkutano wa hadhara, Mhe Mbunge ameshuhudia mechi ya fainali ya Mpira wa Miguu kati ya MsingiMbio na Hatumfosi mtu ambapo pia aligawa zawadi na kuahidi kuwaongezea washindi seti tatu za jezi za mpira.
Katika ziara hiyo Mhe. Ummy aliambatana na Kamati ya Siasa ya Wilaya na Sekretatieti wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Tanga Meja Mst. Hamisi Mkoba na Katibu Ndugu Selemani Sankwa, Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Mhe. Abdurahaman Shiloo, Naibu Meya Mhe. Rehema Mhina, Diwani wa kata ya Maweni Mhe. Joseph Colvas, waheshimiwa madiwani wa kata mbalimbali na viti maalumu.