Komredi Kawaida tarehe 14 Agosti, 2023 amewasili Wilaya ya Mfenesini Magharibi Unguja akiambatana na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika Mikoa ya Zanzibar.
Komredi Kawaida akiambatana na ujumbe wake amewataka na kuwaomba Vijana wa Kitanzania kutumia maarifa yao kujikomboa katika dimbwi la kudanganywa na watu ambao hawaitakii mema Serikali yetu ya awamu ya Sita, richa ya Serikali yetu imejitahidi kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha inawatumikia wananchi wake katika kuhakikisha inapeleka huduma za kijamii, kutatua na kusikiliza kero za watu wake ambao wameiamini Serikali iwaongoze na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kawaida amesema, "Nawaachia kazi na jukumu kubwa la kumlinda na kumtetea Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wake ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa sababu wana mapenzi mema na nchi yetu na ndio maana leo tunaona mabariko makubwa na mapinduzi ya kimaendeleo yamefanyika chini ya uongozi wao, hivyo ni jukumu letu sisi Vijana wa Kitanzania kuwalinda, kuwaombea na kuwatetea kwa hali yoyote viongozi wetu hawa, na tuache kupotoshwa na watu wasioitakia mema Tanzania yetu ya amani.".
Aidha katika ziara hiyo waliweza kutembelea na kukagua miradi mbalimbali sambamba na kushiriki katika shughuli za ujenzi waTaifa, pamoja na kusikiliza kero zilizokuwa zinawakabili wananchi, ikiwemo kutembelea mradi ujenzi wa Soko jipya la kisasa la Chuini na linalojengwa pamoja na kituo cha Mabasi maalum yaani Bus Terminal uliopo Wilaya ya Mfenesini, mradi huo ambao unagharimu takribani Tsh. Milioni 31 za kitanzania ulioanza mwaka jana mwezi wa kumi na moja, unatarajiwa kukamilika Mwaka huu mwezi wa kumi na moja.
Sambamba na kutembelea na kushiriki katika ujenzi wa Taifa ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya za CCM zitakazokuwa na mgawanyo wa Ofisi za UVCCM, Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Wanawake(UWT), Ofisi hiyo itakayokuwa na ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kubeba takribani watu mia nane 800, Komredi Kawaida amewapongeza uongozi wa CCM Wilaya kwa hatua na jitihada za ujenzi huo wa Ofisi.
Pia, katika ziara hiyo wametembelea Vituo vya madereva Bodaboda na bajaji na kusikiliza kero zao, miongoni mwa kero kubwa kwa madereva hao ni swala la kusumbuliwa ikiwemo kukamatwa na askari jamii sambamba na kudaiwa kukata bima baada ya kukabwa na kuibiwa na abiria, katika hilo Kawaida amesema swala la bima amelichukua na atakwenda kuzungumza na watu wa bima, na swala la askari jamii, barabara ya mbuzini hilo ameuomba uongozi wa Serikali Wilaya kulishughukikia.
Aidha, ziara ya Kamati ya Utekelezaji ikiongozwa na Komredi Kawaida katika Wilaya ya Mfenesini imemalizika leo kwa kuweka bendera za Chama Cha Mapinduzi katika nyumba za Maborozi wa mashina ya CCM, na kuwaomba mabarozi hao kutokuwa na hofu juu ya kundi la Vijana kwa maana wapo kwa ajili ya kuwasaidia kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi muda, ba mazingira yoyote Vijana tupo kukitumikia Chama chetu na kuhakikisha tunatafuta kura za ushindi katika Chaguzi zetu ili 2025 tunyanyuke na ushindi wa kishindo zaidi ya Chaguzi zingine.
Mwisho Komredi Kawaida amewaomba Vijana kuwa mstari wa mbele kukitetea na kukipigania Chama Cha Mapinduzi na kuwasemea Viongozi wao ili Chama Cha Mapinduzi kiendelee kushika dora milele kwa maana kina sifa na vigezo vyote.