Na Mwandishi wetu
Zaidi
ya wanafunzi 700 katika shule ya msingi Kikelelwa iliyopo wilayani
Rombo mkoani Kilimanjaro wamesaidiwa kuondokana na changamoto ya hatari
ya kuambukizana magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu hivyo wamepata
msaada wa kujengewa matundu ya vyoo 18 na benki ya Taifa ya biashara
(TCB) ambapo hapo awali walikuwa wanatumia vyoo chakavu na matundu
machache.
Akizundua vyoo hivyo shuleni
hapo Mkurugenzi wa Hazina Tanzania Commacial Bank Wenceslaus Fungamtama
kwa niaba ya Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi
amesema lengo la kujenga vyoo hivyo ni ili kuboresha mazingira na
utulivu wa kujifunza kwa wanafunzi hao wawapo shuleni na wasikumbane na
changamoto ya magonjwa ya kuambukizana.
"Ili
kuunga jitihada za serikali za kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya
na elimu, benki ya TCB hutenga kiasi cha zaidi ya milioni milioni 300
kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimeweza kujenga madarasa, nyumba za
walimu na vyoo katika maeneo mbali hapa nchini" amesema Fungamtama.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Charles Amos ameshukuru benki hiyo kwa kusaidia
ujenzi wa matundu ya vyoo kwani mesema kutokana na uchache wa matundu
ya vyoo yaliyokuwepo awali wanafunzi walilazimika kupanga foleni ya
kusubiriana huku wale wadogo kujikojolea.
"Tunawatoto
waliokuwa wanatoroka kwenda nyumbana kwa aibu ya kujikojolea, hasa muda
wa mapumziko ambao wanatoka darasani kwa pamoja, lakini sasa kwa vyoo
hivi ni wazi kutakuwa na utulivu wa kujifunza" amefafanua Mwl.Amos
Dada
mkuu wa shule hiyo Careen Jonas ameonyesha furaha yake kuwa licha ya
vyoo hivyo kujengwa kisasa, vikizingatia miundombinu ya walemavu lakini
pia vina chumba maalumu cha kubadilishia nguo kwa waschana wawapo kwenye
siku zao za hedhi.
Kwa upande
wake Afisa elimu idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Rombo
Alice Makule, amesema hivi sasa shule inajumla ya wanafunzi 768,
wavulana 385 na wasichana 378 ambapo kwa uwiano ilitakiwa kuwe na
matundu 16 kwa wavulana na 19 kwa wasichana lakini wakitumia matano
matano tu hivyo ujio wa benki hiyo kujenga matundu 18 umepunguza tatizo
kwa kiasi kikubwa.
Shule ya
msingi Kikelerwa ambayo ipo mpakani mwa Tanzania ni moja kati ya shule
kongwe za Mkoa wa Kilimanjaro, licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki
ikiwemo uchakavu wa madarasa vyoo na uchache wa walimu lakini imeendelea
wa kufanya vizuri kitaaluma kiufaulu.