Rais wa Niger Bazoum aondelewa Madarakani

RAIS wa Niger Mohamed Bazoum ameondolewa madarakani, kwa mujibu wa kundi la wanajeshi walioonekana kwenye televisheni ya taifa hilo la Afrika Magharibi saa chache baada ya kumshikilia katika Ikulu ya Rais siku ya Jumatano.


Akisoma taarifa, Kanali Amadou Abdramane, aliyeketi na maafisa wengine tisa, alisema vikosi vya ulinzi na usalama vimeamua: "Kukomesha utawala (wa Rais Bazoum) kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama na utawala mbaya."


Abdramane alisema mipaka ya Niger imefungwa, amri ya kutotoka nje imetangazwa nchini kote, na taasisi zote za jamhuri zimesitishwa.


Wanajeshi hao walionya dhidi ya uingiliaji kati wowote wa kigeni, na kuongeza kuwa wataheshimu ustawi wa Bazoum.


Mapinduzi hayo ya saba katika eneo la Afrika Magharibi na Kati tangu 2020, yanaweza kutatiza zaidi juhudi za Magharibi kusaidia nchi za eneo la Sahel kupambana na uasi wa kijihadi ambao umeenea kutoka Mali katika muongo mmoja uliopita.


Post a Comment

Previous Post Next Post