Disemba 12, 2026, bila shaka itakuwa siku tulivu na yenye pilika nyingi za kiuchumi katika sekta ya utalii duniani, lakini kwa Tanzania, siku hiyo hasa kwa sekta ya utalii nchi yetu itaisimamisha dunia kwa mambo mawili:
Mosi, Tanzania kwa mara ya kwanza katika historia yake itakuwa mwenyeji wa Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards), tuzo za juu zaidi katika sekta hiyo zinazotajwa kuwa sawa na Oscars (katika filamu) na Grammy (katika muziki) au Emmy’s (Katika tasnia ya televisheni).
Pili, kwa mujibu wa taarifa ya jana Oktoba 5, 2026, iliyotolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye makao yake makuu jijini London, Uingereza, Tanzania imeteuliwa kuwania (nominated) takribani tuzo 24 ikijumuishwa na sekta binafsi huku 9 zikiwa zile kubwa za nchi.
Tanzania imeteuliwa kuwania miongoni mwa Tuzo kubwa na za juu mbili yaani Tuzo ya Nchi Bora kwa Ujumla Kiutalii Duniani (World’s Leading Destination 2026) na ile ya Nchi Bora Duniani kwa Utalii wa Safari (World’s Leading Safari Destination 2026). Tuzo ya Safari Tanzania imekuwa tukiitwaa mfululizo kwa miaka minne sasa zikionesha mafanikio ya dhahiri ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tuzo kuu 9 ambazo nchi na vivutio vyake vya Bara na Zanzibar tutawania ni:
1. World's Leading Destination
2. World's Leading Safari Destination
3. Tanzania Tourist Board - World's Leading Tourist Board
4. Serengeti National Park - World's Leading National Park
5. Ngorongoro, Mount Kilimanjaro and Selous Game Reserve - World's Leading
Tourist Attraction;
6. Mpanga-Kipengere Game Reserve and Kitulo National Park World's Leading;
Honeymoon Destination
7. Zanzibar - World's Leading Beach Destination;
8. Zanzibar - World's Leading Island Destination,
9. Zanzibar - World's Leading Festival & Event.
Jinsi ya kupiga kura ingia: https://www.worldtravelawards.com/vote
