Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. Angellah Kairuki, leo Jumatatu tarehe 5 Oktoba 2026 amemkabidhi pikipiki aina ya Boxer Polisi Kata wa Goba, Afande Mwalukuta, ili kumwezesha kuihudumia jamii kwa ufanisi zaidi.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mbunge iliyopo Luguruni, Jimbo la Kibamba, Dar es Salaam.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mhe. Kairuki tarehe 29 Septemba 2026 alipokutana na vijana wa bodaboda na bajaji wa Kata ya Goba. Katika kikao hicho, vijana hao walimuomba Mbunge kumpatia Polisi Kata huyo usafiri, kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri anayoifanya kupitia mpango wa Polisi Jamii.
Pikipiki hiyo inatarajiwa kumsaidia Afande Mwalukuta kufika kwa haraka katika matukio, kufanya doria za mara kwa mara na kuwafikia wananchi wa maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Wananchi wa Goba, hususan vijana wa bodaboda na bajaji, wamepokea hatua hiyo kwa furaha, wakiona kuwa ombi lao limesikilizwa na kutekelezwa kwa wakati.
Ushirikiano huu kati ya Mbunge, Jeshi la Polisi na wananchi unatarajiwa kuimarisha zaidi ulinzi na usalama katika Kata ya Goba
