MAJALIWA AZINDUA RASMI KILI INTERNATIONAL MARATHON 2027


Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amezindua rasmi Kilimanjaro International Marathon 2027, kuelekea maadhimisho ya mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.

Uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Serena, umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi, wakiwemo wadhamini wakuu wa mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager, kampuni ya Yas pamoja na Benki ya CRDB, inayodhamini mbio za kilomita tano (KM 5).

Kilimanjaro International Marathon 2027 inatarajiwa kufanyika Februari 7, 2027, jijini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa riadha, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo na kuitangaza Tanzania kupitia utalii wa michezo.

Mashindano hayo yameendelea kuwa jukwaa linalowakutanisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi, huku yakichangia kuitangaza Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kama kitovu cha matukio ya riadha na utalii nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post