WANANCHI SOMANGA WAMPOKEA AWESO USIKU,ATOA MPANGO WA DHARURA


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kutoa shilingi milioni 500 ili kuanzia jumatatu kuanze kuchimbwa visima Saba katika eneo la Somanga, kilwa Masoko Mkoani Lindi.

Akizungumza na wananchi wa Somanga walojitokeza barabarni usiku kumlaki Waziri Aweso wakati akiendelea na ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa  miradi ya maji, Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe. Kinje kinjikitile alimuomba waziri Aweso kuchimbwa kwa visima sita katika eneo Hilo la Somanga.

" Mhe.Mbunge umeomba vichimbwe  visima sita, sasa Mimi nakuongezea vitachimbwa Saba, Nikuagize Katibu Mkuu kufikia jumatatu hakikisha umeleta milioni 500 hapa Somanga na visima Saba vianze kuchimbwa ili kuongezea nguvu visima vilivyopa na  wananchi wa Somanga wapate huduma ya maji bila usumbufu wowote" Amesema Waziri Aweso

Post a Comment

Previous Post Next Post