Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi Peter Mwasalyanda amekutana na wadau wa Mawasiliano ikiwa makampuni ya Simu, Viongozi wa serikali, Madiwani na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama tarehe 07 Septemba 2026 katika Wilaya na Kilombero.
Kwa mujibu wa Ripoti ya hali ya sekta ya Mawasiliano ambazo kwa robo mwaka inayoishia juni 2026 imeonesha mji wa Ifakara kuongoza kwa kuwa na majaribio ya ulaghai 1,781 kutokea mjini hapo.
Kikao hicho kimejadili jinsi ya kudhibiti matukio ya kihalifu yanayofanywa na matapeli wanaojulikana kama “Halo Halo”. Baadhi ya wazazi wachache wa wilaya ya Kilombero wameonekana kushiriki kusajili laini za simu kwaajili ya kupata kipato na baadae kuingia kwenye matatizo ya kijinai, pale laini zao zinapotumika katika uhalifu.
Wadau hao wamekubaliana kushirikiana kutoa taarifa na kuchukua hatua kwa “Halo Halo” ili kupunguza vitendo vya kitapeli katika mtandaoni.
Katika mkutano huo, Viongozi na Jamii ya wananchi wa Ifakara imeoneshwa umuhimu wa kushiriki katika kuzuia Utapeli kupitia mitandao, kwa kuhakikisha hawaruhusu laini zao kutumika na watu wengine katika vitendo vya uhalifu. Wananchi wengi wameruhusu kuwasajilia laini za simu watu wengine, kwa kupatiwa kipato kidogo na baadae laini hizo kutumika katika vitendo vya utapeli. Wananchi wamekumbushwa kuendelea kuhakiki laini zao za simu kupitia *106# , kukemea tabia hizo katika jamii , kuripoti vitendo vya uhalifu kwa kutuma namba ya tapeli Kwa ujumbe mfupi kwenda 15040 (BURE), kutoa taarifa mara moja pale simu itakapopotea au kuibiwa na pia kutokutoa ushirikiano na mtu yeyote anayedai ni mtoa huduma pasipo kutumia Namba 100, kama siyo namba 100 ni tapeli.
#tcratz #fursasana #usalamamtandaoni
