Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndg Rabia Abdalla Hamid leo tarehe 25/09/2026 ameendelea na ziara ya CCM ya kusikiliza, Kuzungumza na kutatua changamoto za wananchi wa makundi mbalimbali ya kijamii ndani ya Mkoa wa Tabora ambapo amekutana na kuwasikiliza wananchi waliojitokeza kuwasilisha changamoto zao za makundi ya kijamii.
Aidha, Ndg Rabia pamoja na kuwasikiliza wananchi changamoto mbalimbali zinazowakabili, ametumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi wa Mkoa wa Tabora kuwa, Ilani ya CCM 2025-2030 ni jumuishi kwa makundi yote ya kijamii, CCM itatekeleza kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni mtekelezaji wa ahadi anazotoa kwa wananchi wa makundi yote ya kijamii, kila kundi lina umuhimu katika kuleta maendeleo Endelevu kwa watu.
Tags
Siasa
