KITUO CHA KISASA UTALII KUSINI KUKAMILIKA IRINGA DISEMBA


Kituo cha kisasa kinachotarajiwa kuwa mkombozi wa utalii katika Ukanda wa Kusini kimefikia asilimia 88 na kitakamilika Disemba mwaka huu.

Akikagua ujenzi huo leo Septemba 30, 2026, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, ameeleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika mradi huo utakaokuwa na ofisi za wadau wote wa utalii, kumbi za mikutano na huduma za kisasa ikiwemo ngazi ya umeme (escalator). 

“Ujio wa jengo hili unafuatia pia kukamilika kwa jengo jingine la masuala ya utafiti, na jana tumeona uwanja wa ndege Mikumi unamaliziwa lakini pia Iringa kule Ruaha viwanja viwili vya ndege, hostels na majengo mengine pia vilishakamilika lakini pia kuna miradi inaendelea kule Kitulo na Katavi. 

Kwa ufupi Serikali ya Awamu ya Sita ipo kazini katika kuendeleza utalii Kusini,” alisema Dkt. Abbas

Post a Comment

Previous Post Next Post