DUA MAALUM YA AL MARHUM MZEE HAFIDH AMEIR HASSAN YAFANYIKA TANGA


Dua ya Al Marhum Mzee Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, imefanyika  Jumapili, Septemba 13, 2026, katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tanga, baada ya Swala ya Maghrib.

Dua hiyo imehudhuriwa na waumini, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi, kwa ajili ya kumuombea marehemu na kumkumbuka kwa dua na matendo mema.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Dua hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ambaye ameungana na waumini katika kumuombea Al Marhum Mzee Hafidh Ameir Hassan.

Katika dua hiyo, waumini wamemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe marehemu makosa yake, amrehemu, amjaalie mahali pema Peponi na kuipa familia, ndugu na jamaa zake moyo wa subira na uvumilivu. 


Aamiin

Post a Comment

Previous Post Next Post