Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku Musa Bwanku leo Jumanne Septemba 08, 2026 amefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kutoa pole kwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha mume wake Mhe. Hafidh Ameir Hassan.
Ndugu Bwanku alifika Lumumba na kusaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole nyingi sana kwa Rais Samia binafsi pamoja na familia yake huku akimuombea Rais Samia subira na imani kwenye nyakati hizi ngumu za kupoteza mume.
Kwa tangazo la Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, mume wa Rais Samia Mhe. Hafidh Ameir Hassan alifariki Jana Jumatatu Septemba 08, 2026 akiwa anapatiwa matibabu huko hospitali ya Emilio Mzena, Zanzibar na kuzikwa huko Kizimkazi, Zanzibar Jana.
