Mkandarasi anaetekeleza Mradi wa Maji wa vijiji Nane Ngorongoro ametakiwa kuhakikisha ndani ya miezi mitatu Mradi huo umekamilika na unaanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijiji vya Ng'arwa,Mageri, Tinanga, Olorieni, Magaiduru,Mgongo,Yasi na Mdito.
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametoa maagizo hayo wakati alipotembelea kukagua utekelezaji wa mradi huo katika Kijiji cha Yasi.
" Huu Mradi ninaujua vizuri sana, sasa miezi mitatu inawatosha kuhakikisha Mradi huu unakamilika na wananchi wanaanza kupata huduma ya maji" Waziri Aweso amesema
Mradi wa Maji wa vijiji Nane unaotekelezwa na RUWASA pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Arusha (AUWSA) kutoka vyanzo vya Mto Orkanjor na chemchem ya Yasi unathamani ya shilingi bilioni 6.1 na umefikia asilimia 60 ya utekelezaji wake, ukikamilika unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wapatao 32, 000 Mifugo 10,000 waliopo katika vijiji hivyo.
