WATENDAJI MALIASILI NA ITALII WAFANYA ROYAL TOUR NYERERE


Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Agosti 4, 2026, wamemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutangaza utalii aliposhiriki filamu ya “Tanzania: The Royal Tour,” kwa wao nao kufanya ziara ya kitalii Hifadhi ya Nyerere.

Wakiwa mwishoni mwa kikao chao cha siku tatu cha kimkakati kilichohitimishwa kwa hotuba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamad Chande; awali mapema asubuhi watendaji hao kutoka Wizara makao makuu na taasisi zote chini ya Wizara, walifanya utalii wa ndani ili kuitangaza hifadhi hiyo.

“Katika ‘Royal Tour’ yetu ya leo tumeweza kujionea na tuko tayari kulitangaza zao jipya la utalii wa boti unaompa mgeni fursa ya kutalii akiwa kwenye maji ili kujionea viumbe mbalimbali na pia akipata utulivu. 

“Safari ya boti kwenye Mto Rufiji unaopita katikati mwa Hifadhi za Nyerere na Pori la Akiba la Selous, mbali na kutoa fursa ya kuona wanyama, viumbe na mazingira mazuri ya aina mbalimbali, lakini hii ndio moja ya tofauti kubwa kati ya Hifadhi hii na nyingine,” anasema Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara aliyeongoza Royal Tour hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post