Vyombo vya habari vya Ulaya vimeanza kuipa uzito hatua ya Serikali ya Tanzania kuunda Tume ya Jaji Shabani Ally Lila kuchunguza kwa kina watu wanaoweza kuwajibika kwa vurugu zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Ripoti hizo zimeeleza tume hiyo kama hatua inayolenga kuondoa mijadala ya kisiasa na kurejesha uchunguzi kwenye ushahidi, sheria na uwajibikaji.
Kinachovutia zaidi ni namna Indegazette.be ya Ubelgiji https://www.indegazette.be/zes-onafhankelijke-rechters-krijgen-opdracht-verantwoordelijken-voor-tanzaniaans-verkiezingsgeweld-te-identificeren/ na The News Agency yenye makao yake Brussels https://www.thenewsagency.net/news/six-independent-judges-have-been-ordered-to-identify-those-responsible-for-tanzanian-election-violence/ vilivyoangazia muundo wa tume hiyo yenye majaji kutoka Tanzania, Namibia na Uganda, wakieleza kuwa uzoefu huo mpana unaweza kusaidia kujenga uaminifu katika mchakato.
Hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan imeonyesha wazi kwamba Tanzania haikwepi kuchunguza yaliyotokea—imechagua taasisi, sheria na ushahidi kutafuta majibu.
