TANZANIA YAIBUKA MSHINDI KATIKA MASHINDANO YA HISABATI DUNIANI (IMO2026)


Wanafunzi walioshiriki mashindano ya Hisabati ya AFRIKA (PAMO) na ya DUNIA (IMO) Sasa wamerejea na Ushindi, Uwanja  wandege Julius Nyerere International Airport, jijini Dar es Salaam Tarehe 31 Julai 2026. 

Mwanafunzi wa Tanzania, Lightness Ngiliule (wa pili kutoka kushoto), ameibuka mshindi wa kwanza kwa wasichana kutoka Afrika katika Mashindano ya Dunia ya Hisabati (International Mathematical Olympiad – IMO 2026) yaliyofanyika Shanghai, China.

Pamoja na wanafunzi wenzake Angel Zalwango, Sweetbert Nene, Nyandahu Leonard, Joyce Sulumo na Arqam Salim wameipeperusha bendera ya Tanzania vizuri katika mashindano hayo yaliyohusisha nchi 118 kutoka mabara mbalimbali, ikiwemo nchi 15 za Afrika.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inameendelea kutambua na kushirikiana na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) kila mwaka katika kuhamasisha kuhamasisha na kufadhiri ushiriki wa wanafunzi wa Tanzania katika mashindano haya. Hii imechangia Tanzania kuendelea kung’ara na kutambulika kimataifa kwenye ufanisi wa taaluma ya somo la Hisabati. Matokeo haya mazuri ni fursa kwa nchi yetu kuwa sehemu ya maendeleo ya Dunia katika nyanja za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM), pamoja na kushiriki kikamilifu na kunufaika na uchumi wa kidijiti unaotegemea TEHAMA.

Post a Comment

Previous Post Next Post