Kupitia ufadhili wa The Big Heart Foundation, ZMBF imefanya zoezi la ugawaji wa nanga za asili (local anchors) kwa wakulima wa mwani kutoka Shehia za Uzi na Muungoni, chini ya Mradi wa Seaweed Social Enterprise Project (SESEP).
Nanga hizo ni sehemu ya pembejeo bora zinazolenga kuboresha mbinu za ukulima wa mwani, kupunguza uharibifu wa mazao baharini, na kuongeza tija kwa wakulima.
Mradi huo, katika awamu yake ya majaribio, unawanufaisha wakulima 200, wakiwemo wanawake 175 (88%) na vijana 51 wenye umri wa miaka 15–35, kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi kupitia kilimo endelevu cha mwani na kufikia masoko ya ndani na kimataifa.
