RAIS SAMIA AMPOKEA RAIS TSHISEKEDI ZANZIBAR, KUKAZIA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA DRC


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempokea Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, katika Ikulu Ndogo ya Zanzibar.

Mapokezi hayo yanaakisi uhusiano wa muda mrefu wa kirafiki na kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na dhamira ya viongozi hao kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kwa manufaa ya wananchi wa mataifa yote mawili.

Mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa ya viongozi hao kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi ya pamoja, ikiwemo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara, uwekezaji, miundombinu, usafirishaji na masuala ya kikanda.

Ujio wa Rais Tshisekedi nchini Tanzania pia unaendelea kudhihirisha nafasi muhimu ya Tanzania katika kukuza diplomasia, amani, usalama na ushirikiano wa kikanda, hususan katika eneo la Maziwa Makuu na Bara la Afrika kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post