MBUNGE MAVUNDE AANZISHA UJENZI WA ZANAHATI MTAA WA MCHEMWA,MAKUTUPORA-DODOMA



Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde kwa kushirikiana na wananchi wa mitaa ya Mchemwa,Azimio na Mbande kata ya Makutupora ameanzisha ujenzi rasmi wa Zahanati ambayo inalenga kuhudumia zaidi ya wananchi 10,000 wa mitaa hiyo mitatu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kuchimba msingi wa ujenzi wa jengo la zahanati,Mbunge Mavunde amesema tukio hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya kusogeza huduma ya afya karibu na wananchi.

“Ni imani yangu hatua ya leo ya kuanza ujenzi wa zahanati hii itasaidia kutatua changamoto ya muda mrefu ya wananchi wa mitaa hii mitatu kufuata huduma za afya eneo la mbali ya makazi yao.

Tuna imani kubwa na serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan juu ya kutuunga mkono na kukamilisha ujenzi wa zahanati hii.

Pamoja na kununua eneo la ujenzi wa Zahanati hii kwa Tsh 6,000,000,lakini pia nitachangia matofali 5000 na saruji mifuko 250”Alisema Mavunde

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi,Diwani wa Kata ya Makutupora ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Jiji La Dodoma Mh. Almon Chaula amemshukuru Mh. Mavunde kwa kutimiza ahadi yake ya kuanzisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itasaidia kutatua changamoto za huduma za Afya katika maeneo hayo na kutoa rai kwa wananchi kuunga mkono juhudi hizi kwa kuchangia nguvu kazi wakati wa ujenzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post