Nyerere ni jina ambalo wiki hii linakwenda kuheshimishwa sana; Mosi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anakwenda kuzindua mradi wa megawati 2,115, ndoto kuu ya Mwalimu na suluhisho la changamoto za umeme nchini.
Pili, Je, wajua?? Mradi huo upo ndani ya Hifadhi yenye jina la Mwalimu tena; Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.
Sasa sikia zaidi ya hapo. Kama umeona tangu jana na leo au walau umesikia wageni wengi wametua mahali flani hivi amazing kuelekea uzinduzi huo wakimemo wale wanaoendelea kutalii.
Kwa mfano umeona leo hata ndege ya Bombardier Q400 ya ATC imetua Hifadhi ya Nyerere kupitia uwanja huo mpya wa kisasa wa Mtemere unaoleta mageuzi makubwa katika utalii nchini.
Sasa sikiliza takwimu hizi:
✍🏽Uwanja huo ni miongoni mwa viwanja vinne vya kisasa vya ndege vya kiutalii vinavyotekelezwa kupitia Mradi wa Serikali ya Awamu ya Sita wa Kufungua Utalii Kusini.
✍🏽✍🏽Kupitia Mradi huo viwanja vitatu vikali kama hiki vimekamilika na kuanza kazi kikiwemo hiki cha Mtemere (Nyerere) na vingine viwili vimeshakamilika kule Hifadhi kubwa nyingine ya Ruaha (kimoja upande wa Iringa kingine upande wa Mbeya). Kiwanja cha nne kinakamilika wakati wowote mwaka huu Hifadhi ya Mikumi, Morogoro.
Hapo Mikumi kama ulimsikia yule Mwenyekiti wa TATO pale Ikulu Mzee Chamburo akisema alifika akakuta ardhi “inafukuliwa” kona zote basi ndio hili “lieapoti” jingine linakuja pale Mikumi kama hili la Mtemere👊🏽 Kazi inaendelea mchana na usiku!!
✍🏽✍🏽✍🏽Kwa taarifa zaidi viwanja hivi ni vya kwanza vya kisasa zaidi kuwahi kutokea nchini na vyenye lami maalum kujengwa katika Hifadhi zetu ikiwa ni maono makuu ya Awamu ya Sita kufungua utalii. Nimesema vina lami maalum. Nitarudi. Utaelewa👇🏽
✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽Turudi uwanja huu wa Mtemere. Una “run-way” ya urefu wa kilometa 1.8 lakini ukijumlisha na maeneo ya “run-way” ya akiba uwanja una jumla ya urefu wa kilometa 2.5 ikiwa na uwezo wa kutua madege makubwa tu yenye abiria wengi jambo ambalo ni mageuzi makubwa sasa kutoka ndege ndogo tulizozoea zikitua Hifadhini hadi madege ya maana;
Pamoja na kituo cha kuongoza ndege, kituo cha zimamoto, ofisi, maeneo ya tiketi na vibanda vya kubarizi, viwanja hivi vya kisasa ikiwemo hiki cha Mtemere vina majengo makali ya kupokea abiria 140 wanaowasili na pia wengine 140 wanaoondoka kwa wakati mmoja.
Ni uwanja wenye “run-way” ya upana wa meta 30 na eneo la wazi lenye meta 120 na ulizinduliwa rasmi kuanza kufanya kazi Februari mwaka huu 2026 ambapo Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alimwakilisha Rais Samia!
Hii ya mwisho sasa ishike vyema: unaona kwenye picha tulizoambatisha hapa kuna “run-way” unaona kama ya udongo hivi😎 Hakuna udongo hapo. Tulia. Jifunze.👌🏽👌🏽
Kwa taarifa yako ule sio udongo. Eneo lote la kutua na kurukia ndege na mpaka maegesho ya viwanja hivi vya ndege vya aina yake unaona kuna rangi nyekundu nasema tena sio udongo ule Mtanzania mwenzangu. Mambo ya teknolojiaaaaa!!
Ile ni lami maalum inaitwa polymer ambayo inaweka tabaka gumu kama lami ya kawaida lakini inachanganywa na udongo na rangi inayoakisi uhalisia wa uhifadhi. Hivyo pale hakuna vumbi wala tone la tope iwe mvua iwe jua madege yanatua tu!
Haya ndio maajabu ya Uwanja wa Ndege wa Mtemere, wa kwanza wa aina yake na ambao leo ndege ya ATC imetua kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya Hifadhi, tukiwa tunaelekea tukio la kihistoria la uzinduzi wa Bwala la Umeme wa Maji la Mwalimu Nyerere!!!👌🏽👏🏼🇹🇿
