TANZANIA YAZINDUA SAFARI ZA MOJA KWA MOJA DAR ES SALAAM–MUSCAT, YAITANGAZA OMAN KUWA SOKO LA KIMKAKATI LA UTALII


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi safari za moja kwa moja za Air Tanzania kati ya Dar es Salaam na Muscat na kuitangaza Sultanate ya Oman kuwa moja ya masoko ya kimkakati ya utalii, hatua inayolenga kuimarisha utalii, biashara na uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili.

Akizungumza leo Julai 26, 2026 katika Jukwaa la Utalii Tanzania–Oman, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande, amesema mafanikio hayo yanatokana na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha muunganiko wa Tanzania na masoko ya kimataifa kupitia usafiri wa anga.

Ameongeza kuwa safari hizo zitachochea ongezeko la watalii, biashara na uwekezaji, huku Tanzania ikilenga kufikia watalii milioni 8 wa kimataifa ifikapo mwaka 2030. 

Mwaka 2025, Tanzania ilipokea watalii wa kimataifa 2,294,495, watalii wa ndani 3,610,960, na kuingiza Dola za Marekani bilioni 4.4 kutokana na utalii.

Aidha, amesema Tanzania ilipokea wageni 15,111 kutoka Oman mwaka 2025, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa kufuatia kuanza kwa safari za moja kwa moja.

“Tanzania haiji Oman kutafuta watalii pekee, bali kujenga ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu utakaoleta manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili, amesema Mhe. Chande.”

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema sekta ya utalii na sekta ya uchukuzi na usafirishaji zinasaidiana ndio maana uzinduzi wa safari ya ndege umeendana na kongamano la wadau wa utalii wa Oman na wenzao wa Tanzania. Zaidi ya makampuni 100 ya Tanzania na Oman yamekutana

Post a Comment

Previous Post Next Post